"Hatubabaishwi na Dkt. Mwinyi Urais Zanzibar"-ACT-Wazalendo

10Jul 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
"Hatubabaishwi na Dkt. Mwinyi Urais Zanzibar"-ACT-Wazalendo

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimejipanga vyema kuibuka na ushindi wa kishindo katika nafasi ya Urais visiwani Zanzibar na kwamba hakibabaishwi na mgombea wa Chama cha Mapinduzi aliyepitishwa na halmashauri kuu ya chama hicho Jijini Dodoma leo,Dkt Hussein Mwinyi.

Akizungumza na The Guardian Digital muda mfupi tu baada ya kupitishwa kwa mgombea wa CCM, Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu ametamba kuwa mgombea waliyemuandaa hawezi kushindwa uchaguzi huo kwa kile alichodai kuwa ana uzoefu wa kutosha katika siasa za Zanzibar.

“Dkt.Hussein mwinyi ni mtu ambaye tunafahamu uwezo wake na udhaifu wake na kwetu sisi ni mgombea ambaye ni dhaifu zaidi kwa hiyo tutapata ushindi mnono” amesema Shaibu

Tayari Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif ameshatangaza kuwa atawania urais katika chama hicho ambapo itakuwa ni mara ya 6 kwa mkongwe huyo wa siasa kuwania Urais katika visiwa hivyo.

 

 
 
 

Habari Kubwa