Hatutashiriki kikao cha Msajili -Zitto

26Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Hatutashiriki kikao cha Msajili -Zitto

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amesema chama hicho hakitoshiriki kikao kitakachofanyika Oktoba 21, mwaka huu kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa, kwa kuwa watakuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Haki, Maridhiano na Amani uliotishwa na TCD.

Zitto Kabwe.

Zitto ameandika hayo leo Septemba 26, katika ukurasa wake wa Twitter ambapo ameambatanisha na barua ya taarifa kwa umma.

“Tulijitahidi kuboresha kikao cha Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa kilichoitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa. Msajili, kwa makusudi, amepanga kikao tarehe 21 Oktoba 2021 siku ya Mkutano wa Kitaifa wa Kituo cha Demokrasia na Tanzania (TCD), ACT Wazalendo tumeamua HATUTASHIRIKI kikao cha Msajili” ameandika Zitto.

Habari Kubwa