HESLB: Waliorejesha mikopo elimu ya juu wafikia 198,656

15Jan 2019
Beatrice Shayo
Dar es salaam
Nipashe
HESLB: Waliorejesha mikopo elimu ya juu wafikia 198,656

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema wamefanikiwa kuwabaini wanufaika wapya 12,600 ambao walikuwa hawajaanza kurejesha na kwa sasa wameanza kurejasha na kufikia idadi ya 198,656 wanaorejesha mikopo yao.

Mkurugenzi mkuu wa heslb, abdul-razaq badru.

Aidha, HESLB imesema itaanza kuwasaka waajiri ambao hawawakati waajiriwa wao asilimia 15 ya mkopo wao ili waweze kupata deni sugu wanalolidai la Sh bilioni 291 kwa wanufaika 100,009.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB,  Abdul-Razaq Badru, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ukusanyaji mikopo katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo wamekusudia kukusanya Sh. Bilioni 150.

Habari Kubwa