H/mashauri zapewa siku 60 ujenzi wa madarasa 62

03Dec 2018
Dege Masoli
Handeni
Nipashe
H/mashauri zapewa siku 60 ujenzi wa madarasa 62

MKUU wa Wilaya ya Handeni, Gondwin Gondwe, amezipa siku 60 Halmashauriza Handeni Mji na Vijijini kukamilisha ujenzi wa vyumba 62 vya madarasa katika shule za sekondari zenye upungufu.

MKUU wa Wilaya ya Handeni, Gondwin Gondwe.

Pia amezitaka na kuhakikisha hakuna atakayeshindwa kuanza kidato cha kwanza mwakani kwa kukosanafasi.

Gondwe alitoa agizo hilo wakati wa kikao maalumu kwa ajili ya kujadili mustakabali wa elimu wilayani humo ambacho kiliwashirikishawadau mbalimbali wa elimu wakiwamo wakuu wa shule, walimuwakuu, waratibu elimu kata na watendaji.

Aliwataka wakurugenzi wa halmashauri hizo kuzingatia maagizo hayo na kwamba yatekelezwe ndani ya siku 60, ili kutokwamisha mpango waserikali wa kutoa elimu bure kwa kila mwenye umri wa kwenda shule kwa kisingizio cha upungufu wa vyumba.Gondwe alizungumzia mkakati wa wilaya wa kuinua elimu kuwa ni pamoja na kujiwekea maazimio 12 yakiwamo kuanzisha mashamba darasa kwa kila shule ili kuondoa tatizo la ukosefu wa chakula kwa wanafunzi.Alitaja baadhi ya maazimio hayo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ni upatikanaji chakula shuleni, kuboresha mazingira ya ufundishaji, miundombinu, vitendeakazi, ufundishaji wa uhakika, ukaguzi, maandalizi ya kazi, motisha na udhibiti wa utoro kwa wanafunzi.Hata hivyo, aliwapongeza walimu wa shulekumi bora kiwilaya na kuwataka wakuu wa shule zilizofanya vibaya kujitathmini na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, William Makufwe, kuangalia namna ya kuzisaidia shule hizo.Katika matokeo ya mwaka huu, Halmashauri ya Handeni Vijijini ilipata asilimia 81 wakati Handeni Mji ni asilimia 73.6, ikiwa ni matunda ya kikaokama hicho nilichokutana mwaka 2017 ambapo matokeo yalikuwa ya asilimia 73 na 78.

Habari Kubwa