Huheso watoa vifaa vya milioni 4 kujikinga na corona kwa wanafunzi

02Jun 2020
Shaban Njia
KAHAMA
Nipashe
Huheso watoa vifaa vya milioni 4 kujikinga na corona kwa wanafunzi

Shirika lisilo la kiserikali la Huheso Foundation lililopo Kata ya Malunga, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, limekabidhi vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa corona kwa wanafunzi wa kidato cha sita venye thamani ya shilingi Milioni 4.6.

MKURUGENZI wa shirika lisilo la kiserikali la Huheso Foundati, Juma Mwesigwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya kahama, Anamringi Macha vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19. PICHA NA SHABAN NJIA

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Mkurugenzi wa Shirika hilo Juma Mwesigwa, amesema,vifaa hivyo vimetolewa kwa ufadhili wa Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS) kama moja ya kupambana na ugonjwa huo kwa wanafunzi hao.

Amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita,vitasaidia kuwakinga wanafunzi hao na ugonjwa wa Covid-19 wakati wote watakapokuwa mashuleni.

Vifaa hivyo vimegharimu kiasi cha Shilingi milioni 4.6 fedha hizo ni kati ya kiasi cha shilingi milioni 30 kutoka kwenye mradi wa baki salama.

Mwesigwa amesema vifaa hivyo ambavyo ni Ndoo za maji 40, Barakoa 150, Sanitizer lita 10 ambazo zimetengenezwa na Ofisi ya Mfamasia wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Sabauni 128.

“Ndugu zangu, tunatoa vifaa hivi vya kujikinga na corona kwa wanafunzi wetu wa kidato cha sita kama moja ya kutekeleza mradi wa baki salama ambao tumefadhiwa na The Foundation For Civili Society,tunaomba vifaa hivi viwafikie walengwa ili viwasaidia kwa kipindi hiki wawapo mashuleni” amesema Mwesigwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha amelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kupambana na kutoa elimu ya kujikinga na Covid-19 na kuongeza kuwa vifaa hivyo vimefika kwa wakati ambapo wanafunzi wanauhitaji na vifaa hivyo.

Habari Kubwa