Idadi ya vifo yaongezeka ajali ya Same

14Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Same
Nipashe
Idadi ya vifo yaongezeka ajali ya Same

Idadi ya vifo vilivyotokea katika ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro vimeongezeka na kufikia 11 baada ya majeruhi mmoja kati ya saba waliolazwa Hospitali ya Wilaya ya Same kufariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule, amesema hali za majeruhi wawili kati ya sita siyo nzuri na wamekimbizwa katika katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku wanne hali zao zinaendelea vizuri baada ya majibu ya X-ray kuonyesha wamepata majeraha madogo madogo.

Ajali hiyo ilitokea jana wilayani Same ambapo magari mawili yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na majeruhi 12 kati ya hao sita walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same na wengine saba Hospitali ya KCMC.

Habari Kubwa