IGP Sirro: Matukio ya ubakaji yamekithiri nchini

01Mar 2019
Mary Geofrey
Dar es Salaam
Nipashe
IGP Sirro: Matukio ya ubakaji yamekithiri nchini

MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini, Simon Sirro, amesema licha ya matukio ya uhalifu wa kutumia silaha na biashara za dawa za kulevya kupungua nchini, matukio ya ubakaji yamekithiri.

MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini, Simon Sirro.

Amesema Jeshi la Polisi, limejipanga kukabiliana nayo kwa kuanza kutoa elimu kuanzia shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu ili kuepuka tatizo hilo.

Sirro aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maofisa waliopandishwa vyeo na Rais John Magufuli na mabadiliko madogo ya watendaji wake aliyofanya.

“Sababu kubwa ya kukithiri kwa matukio haya ni mmomonyoko wa maadili. Licha ya adhabu kali zinazotolewa kwa watuhumiwa wa matukio haya.

Jeshi la Polisi limejipanga kutoa elimu kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu, kubandika na matangazo yanayoelezea madahara ya matukio ya ubakaji," alisema IGP Sirro.

Pia aliwaasa viongozi wa dini na wanasiasa kuanza kutoa elimu kwa jamii kukabiliana na tatizo hilo ambalo linakatisha ndoto za watoto wa kike.

Habari Kubwa