IGP Sirro aonya wanaojipanga kufanya fujo uchaguzi mkuu

03Jul 2020
Dotto Lameck
Arusha
Nipashe
IGP Sirro aonya wanaojipanga kufanya fujo uchaguzi mkuu

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, ametoa onyo kwa watu wanaotegemea kufanya fujo kipindi cha uchaguzi mkuu na kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro.

Sirro amesema hayo wakati akizungumza na maofisa wa Jeshi hilo jijini Arusha, huku akiwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi utakwenda vizuri kama ilivyopangwa na jeshi hilo litatenda haki kwa kila mmoja.

Aidha, Sirro amesema askari wa Jeshi hilo tayari wameshapatiwa mafunzo ya kutosha yatakayowawezesha kukabiliana na vitisho mbalimbali ikiwemo uhalifu na wahalifu pamoja mbinu nyingine za kuwashughulikia watakaovunja sheria, huku akiwataka askari hao kuendelea kutoa elimu kwa wananchi.

Habari Kubwa