'Iron Dome' mfumo wa Israel kujilinda na Makombora

15May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
'Iron Dome' mfumo wa Israel kujilinda na Makombora

Ufyatulianaji wa makombora kati ya vikosi vya Israel na wapiganaji wa Palestina unaendelea huku Umoja wa Mataifa ukihofia 'vita vikali vaidi'.

Tangu Jumatatu, Wapiganaji wa Hamas wamerusha makombora 1000 katika ardhi ya Israel mengi yakilenga mji mkuu wa Tel Aviv na maeneo yake nao wanajeshi wa Israel wakifanya mashambulizi ya mabomu katika ukanda wa Gaza na kuwauwa makumi ya raia.

Lakini Israel ina kinga yenye uwezo mkubwa kujilinda dhidi roketi zinazorushwa na Hamas kutoka Gaza , kwa jina 'Iron Dome'.

Kama ilivyoripotiwa na jeshi la Israel, kati ya roketi 1050 zilizorushwa, 850 zilitunguliwa na mfumo huo wa kutungua makombora.

Habari Kubwa