Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo, amesema atawasilisha majina ya Wakurugenzi hao kwenye mamlaka yao teuzi kwa ajili ya hatua stahiki.
"Kwakuwa Wakurugenzi wa Halmashauri Mamlaka yao ya Uteuzi ni Rais, nitawasilisha majina yao ili wachukuliwe hatua kwa kadiri atakavyoona inafaa," amesema Jafo.
Aidha, Waziri Jafo amewataka watendaji wote katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kuchapa kazi kwa uadilifu kwa lengo la kuwatumikia wananchi.