Jafo ampa maagizo mazito Katibu Mkuu TAMISEMI

01Nov 2020
Julieth Mkireri
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Jafo ampa maagizo mazito Katibu Mkuu TAMISEMI

WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Joseph Nyamhanga, kutoa maelekezo kwa waganga wakuu wa mikoa kuwapa ushirikiano wanafunzi wa taaluma ya udaktari wanaokwenda kupata mafunzo kwa vitendo.

Jafo alitoa agizo hilo juzi wakati akiweka jiwe la msingi katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha City, Tawi la Chanika.

Alitoa agizo hilo baada ya kupokea maelezo ya vikwazo vinavyowakabili wanafunzi wa chuo hicho wanapokuwa katika mafunzo kwa vitendo kutoka kwa uongozi wa chuo hicho.

Waziri Jafo alimtaka Katibu Mkuu Nyamhanga kuhakikisha anatoa maelekezo hayo mapema ili wanafunzi wanapokwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye hospitali na vituo vya afya, wapewe ushirikiano na usimamizi wa kutosha.

"Hawa wanafunzi wanatakiwa kupewa ushirikiano kwenye maeneo wanayokwenda ili hata wanapopata ajira wawe wamekamilika kwa nadharia na vitendo," alisema............kwa habari zaidi fuatilia epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa