Jafo atokwa na machozi kisa ukosefu huduma za afya

03Aug 2020
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Jafo atokwa na machozi kisa ukosefu huduma za afya

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, amejikuta akitokwa na machozi akizungumzia namna wananchi walivyokuwa wakipata adha na kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa huduma za afya kwenye baadhi ya maeneo nchini.

Hali hiyo ilimkumba leo alipokuwa akizungumza kuhusu mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma ya afya ya msingi chini ya ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Tamisemi’ iliyofanyika Jijini Dodoma.

Amesema wananchi wengi walikuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma za afya, lakini kwa kipindi cha miaka mitano serikali chini ya Rais John Magufuli imetoa kipaumbele kwa sekta hiyo na kuondoa adha kwa wananchi.

“Kuna watu wenye uwezo hawafahamu kwamba watanzania walikuwa wanateseka, walikosa kupata huduma za afya, na wanasafiri zaidi ya kilometa 140 kufuata huduma za afya, kina mama wanapata matatizo ya fistula, baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu na vituo vipo mbali,”amesema.

Habari Kubwa