Jaji Mkuu aonya uanaharakati TLS

25Apr 2018
Hellen Mwango
Nipashe
Jaji Mkuu aonya uanaharakati TLS

JAJI Mkuu Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amekitaka Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kuacha uanaharakati na badala yake kisimamie misingi na kanuni za taaluma yao ikiwamo kuishauri serikali, mahakama na bunge.

Kadhalika amekitaka TLS kuacha kulumbana kupitia vyombo vya habari kwa kuwa ni taasisi iliyoanzishwa kisheria lakini imepewa majukumu ya kufanya kazi ya umma.

Rai aliitoa jana o sini kwake, jijini Dar es Sa- laam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhalali wa chama hicho kwamba ni taasisi ya umma kutokana na kupewa jukumu la kuishauri masuala ya kisheria serikali, mahakama, bunge pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa Watanzania.

“Nawashauri viongozi wapya wa TLS waache uanaharakati na kwamba wanatakiwa kushirikiana na Mahakama katika masuala ya kisheria kwa umma badala ya kulumbana kwenye magazeti au vyombo vya habari. Malumbano kupitia vyombo vya habari hayawasaidii wanasheria,” alisema na kuongeza:

“TLS imeanzishwa kisheria kama taasisi bin- afsi lakini imepewa majukumu ya kufanya kazi ya umma ikiwamo kutoa msaada wa kisheria kwa Watanzania.”

Akifafanua zaidi alisema mawakili wote ili kupata uanachama lazima wapitie Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) au vyuo vikuu vinavyotoa shahada ya sheria pamoja na shule ya sheria (Low School), mtiririko huo kupitia vyombo vya umma ni wazi kuwa TLS si taasisi binafsi bali ni ya umma.

Alisema chama hicho kitimize majukumu ya umma ikiwamo kuisaidia serikali, mahakama na bunge nchini. Mapema Aprili 20, mwaka huu, Ikulu jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu alitamka mbele ya Rais Dk. John Magufuli kwamba TLS ni taasisi ya umma baada ya kuulizwa kama ni taasisi binafsi au ya umma. 

Habari Kubwa