Jaji Mwaimu ateuliwa M/kiti wa Tume Haki za Binadamu

23Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Jaji Mwaimu ateuliwa M/kiti wa Tume Haki za Binadamu

RAIS John Magufuli amemteua Jaji mstaafu Mathew Mwaimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa sambamba na uteuzi wa Mwenyekiti, Rais Magufuli pia amemteua Mohamed Khamis Hamad (Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar) kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Vile vile, ameteua makamishna watano wa tume hiyo ambao ni Dk. Fatma Rashid Khalfan (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar), Thomas Masanja (Mhadhiri wa Sheria, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino – SAUT), Amina Talib Ali (Ofisa Mwandamizi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Khatib Mwinyi Chande (Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT) na Nyanda Josiah Shuli (Ofisa Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango).

Taarifa hiyo imesema uteuzi huu umeanza Septemba 19.

Habari Kubwa