Jakaya Kikwete amlilia Bendera

07Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Jakaya Kikwete amlilia Bendera

Waziri wa Habari Mstaafu na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mstaafu, Joel Bendera amefariki dunia jioni ya jana Disemba 6 katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

 Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Muhimbili , Aminiel Eligaeshi alisema  walipomkea Bendera majira ya saa 12:24 Mchana  akitokea Bagamoyo na amefariki  saa 4:03 jioni ambapo chanzo cha ugonjwa wake hakijawekwa wazi. 

Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mkuu wa Mkoa mstaafu, Dk. Joel Bendera nyumbani kwa marehemu Sinza, Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mkuu wa Mkoa Manyara mstaafu, Dk. Joel Bendera, nyumbani kwa marehemu Sinza, Dar Es Salaam.

 

Mbunge wa Jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu mstaafu,Mhe. Philipo Mulugo, akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mkuu wa Mkoa mstaafu, Dk. Joel Bendera, nyumbani kwa marehemu Sinza, Dar Es Salaam.

Habari Kubwa