Jamhuri yaibua mapya ushahidi kesi ya Mbowe

14May 2019
Hellen Mwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Jamhuri yaibua mapya ushahidi kesi ya Mbowe

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa na shahidi wa kwanza wa Jamhuri katika kesi kufanya mkusanyiko isivyo halali inayomkabili Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),-

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe na wenzake wanane kuwa askari polisi walifyatua risasi zaidi ya 90 kuzuia waandamanaji wa chama hicho.

Shahidi huyo ambaye ni Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi, Gerald Ngichi, alitoa madai hayo jana wakati akihojiwa na wakili wa utetezi, John Malya, kutaka kufahamu idadi ya risasi zilizofyatuliwa.

Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Ngichi alidai waandamanaji walikuwa zaidi 500 na waliokamatwa ni waandamanaji 43 ambapo hakuna aliyeangukiwa na risasi.

Mahojiano ya wakili wa utetezi Malya na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:

Mallya: Shahidi kati ya waandamanaji mliowakamata miongoni mwao kuna mliowakuta na silaha?

Shahidi: Hapana.

Mallya: Je, askari uliowaamrisha kupiga risasi za moto hewani walitumia silaha ya aina gani?

Shahidi: Ak47.

Mallya: Shahidi risasi ya aina hiyo ya bunduki ikipigwa inakwenda wapi?

Shahidi: Inaenda hewani, halafu inarudi chini.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Salum Mwalimu; Mbunge wa Kibamba, John Mnyika; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.Katika kesi hiyo jopo la mawakili wa serikali linaongozwa na Faraja Nchimbi, Paul Kadushi, Wankyo Saimon na Jacline Nyantori.  Jopo la Mawakili wa utetezi linaongozwa na Prof. Abdalh Safari, Peter Kibatala, John Malya, Hekuma Mwasipu na Jeremiah Ntobesya.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo kula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali.

Habari Kubwa