Jamii yahimizwa kusaidia watoto wakati wote

10Apr 2017
Rahma Suleiman
Zanzibar
Nipashe
Jamii yahimizwa kusaidia watoto wakati wote

JAMII imeombwa kuwaangalia watoto wanaopatwa na misukosuko ya maisha kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili, badala ya kuwalaumu kwa kuwatolewa maneno ya kashfa na udhalilishaji.

Mkurugenzi wa Zafela, Jamila Simai.

Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zafela) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (Tamwa) ofisi ya Zanzibar, wamesema kufuatia kuenea kwa mitandao ya kijamii, haki nyingi za wanawake na watoto zinavunjwa kupitia mitandao hiyo.

Mkurugenzi wa Zafela, Jamila Simai, alisema jamii inapaswa kuwalea na kuwasaidia
watoto hadi wanapopatwa na majanga mbalimbali, yakiwamo kupewa ujauzito, kubakwa,
kutelekezwa na kutaka kujitoa roho zao wenyewe.

“Watoto ni taifa la kesho hivyo, jamii haina budi kusimama imara kuhakikisha kuwa wanakuwa katika matarajio ya jamii ili kuweza kujitegemea wenyewe na kusaidia taifa kwa ujumla,” alisema Dk. Simai.

Naye Mratibu wa Tamwa Zanzibar, Dk. Mzuri Issa, aliishauri Serikali kuweka mifumo madhubuti ya kukabiliana na majanga ya watoto mara tu yanapotokea ili kupunguza athari hasi za watoto hao.

Aliishauri jamii kuweka programu maalum za kuongoza Taifa la kufanya baada ya watoto kupata majanga ili Serikali, familia, wazazi na wanafunzi wajue namna ya kuishi na mtoto aliyepatwa na matatizo.

“Watoto wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu wanapofikwa na majanga yakiwamo ya udhalilishaji na kukosa faraja kutoka kwa jamii kutokana na mifumo yetu kulegea katika sehemu mbalimbali kutoka jamii hadi taifa,” alisema Dk. Mzuri.

Habari Kubwa