Jamii yatahadharishwa ukimwi upo

21Feb 2016
Frank Monyo
Dar
Nipashe Jumapili
Jamii yatahadharishwa ukimwi upo

BARAZA la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (Nacopha) limeitaadhalisha jamii kujilinda dhidi ya maambukizi ya ukimwi na kuondokana na fikra kwamba ugonjwa huo umeisha, kwani bado ni tishio.

Hayo yamezungumzwa na Meneja Ufuatliaji wa Tathimini wa Nacopha, Rachel Jacob wakati wa mafunzo ya watoa huduma ngazi ya jamii, vituo vya afya na maofisa ustawi wa jamii yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Jamii inapaswa kuchukua taadhari kwani maambukizi bado yapo hivyo tunapaswa kubadilika na kuwa na tabia ya kupima VVU (Virusi vya Ukimwi) mara kwa mara ili kujua afya zetu,” alisema.

Alisema kuwa Nacopha wameanzisha mradi wa ‘Sauti yetu’ ambao unawahusisha watu wanaoishi na VVU ili kusambaza elimu kwa jamii ili kukabiliana pamoja na kujikinga na maambukizi hayo.

Kwa upande wa Daktari wa Kituo cha Afya cha Pungu Kajiungeni, Honest Lyimo alisema hali ya maambukizi bado ipo juu huku wanandoa wengi wakiwa hatarini.

“Nilifanya utafiti katika kituo chetu, na kugundua kuwa wanandoa wengi siyo waaminifu na wamekuwa wazito kutumia kinga hata pale wanapotoka nje ya ndoa huku wengi wanakutwa na maambukizi zaidi ya vijana walio nje ya ndoa,” alisema.

Habari Kubwa