Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanae wa kumzaa

23Jun 2022
Na Mwandishi Wetu
Iringa
Nipashe
Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanae wa kumzaa

MAHAKAMA ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu Kumbuka Mhotelwa (30), kifungo cha miaka 30 na fidia ya shilingi milioni moja kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 6.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Emmy Msangalufu, amesema mtuhumiwa amekutwa na hatia ya kutenda kosa hilo Novemba 19, 2020 nyumbani kwake alipokuwa akiishi na mke wake ambaye alikuwa mgonjwa.

Amesema siku ya tukio alishtuka usiku na kukuta mumewe hayupo kitandani na alipotazama sebuleni akamuona mumewe akiwa anambaka mwanae aliyekuwa na umri wa miaka 6 huku pembeni yake kukiwa na Mtoto mwingine mwenye umri wa miaka mitatu na alikuwa macho akishuhudia baba yake akimbaka dada yake.

Baada ya kushuhudia hivyo alipiga kelele kumkataza mumewe asiendelee na tukio hilo lakini haikusaidia kwa sababu mwanamke huyo alikuwa hawezi kusimama na hivyo kushindwa kumzuia kuendelea kumbaka, baada ya kumaliza tukio hilo mtuhumiwa alimtisha mke wake kuwa endapo atasema popote baasi atamuua.

Hata hivyo baada ya kupambazuka mkewe alikwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi ndipo mtuhumiwa akakamatwa na mtoto akapelekwa hospitalini walipothibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa amebakwa kutokana na kuwa na michubuko.

Habari Kubwa