Jenerali Waitara Mwenyekiti Tanapa

31Oct 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Jenerali Waitara Mwenyekiti Tanapa

RAIS John Magufuli, amemteua Jenerali mstaafu, George Marwa Waitara, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, ilieleza kuwa uteuzi huo ulianza Jumamosi.

Jenerali mstaafu Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dk. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI). Kabla ya uteuzi huu Dk. Eligy Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng'ombe Makao Makuu ya TALIRI.

Balozi Kijazi alisema uteuzi wa Dk. Shirima ulianza juzi.

Habari Kubwa