Jeshi la Polisi halitavumilia udhalilishaji wa kidini

14Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
DODOMA
Nipashe
Jeshi la Polisi halitavumilia udhalilishaji wa kidini

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limewaonya viongozi wa dini mkoani humo ambao wana tabia ya kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na mafundisho ya dini na kuwataka viongozi wa dini kuwafichua wanaofanya vitu vya namna hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi, Gilles Murroto.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi, Gilles Murroto amewaambia viongozi wa dini kuwa hawezi kuvumilia vitendo vya namna hiyo kuendelea.

Kamanda Murroto amesema kutokana na utandawazi ulivyo hivi sasa kuna vingi vinafanyika na vimekuwa na madhara kwa jamii hivyo Jeshi la polisi halitavumilia udhalilishaji wa kidini wa namna yoyote ile.

Katika mkutano huo baina ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma na viongozi wa dini,viongozi hao wamemhakikisha Kamanda Murroto kuwa watakuwa vinara wa kufichua vitendo hivyo.

Kamanda Murroto amewaagiza viongozi wa dini kuhakikisha nyumba za ibada wanazoziongoza zinakuwa na ulinzi wa uhakika.

Pia amewaambia viongozi wa dini mkoani humo kuwa ukosefu wa ulinzi katika nyumba za ibada kwa namna moja ama nyingine imekuwa ni kishawishi kwa watu wenye nia ovu kufanya vitendo hivyo vya uhalifu.

 

 

Habari Kubwa