Jeshi la Zimamoto kutatua changamoto ya magari, elimu ya majanga

18Jun 2019
Happy Severine
Bariadi
Nipashe
Jeshi la Zimamoto kutatua changamoto ya magari, elimu ya majanga

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto Kamishina Jenerali, Thobias Andengenya amesema jeshi lake limejipanga kutatua changamoto ya elimu kwa wananchi pamoja na usafiri ili kuwezesha jeshi hilo kufanya kazi ipasavyo.

mkuu wa jeshi la zimamoto kamishina jenerali Thobias Andengenya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani,kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kamishina msaidizi wa zimamoto John James.

Kamishina huyo amesema hayo leo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu ya kukagua kazi na changamoto zinazokikabili jeshi hilo Mkoani Simiyu.

Andengenya amesema kumekuwepo na tatizo la elimu kwa wananchi juu ya kudhibiti na kukabiliana na majanga ya awali ya moto hivyo wao wamejipata kutoa elimu hivyo kwa wananchi sehemu mbalimbali ikiwemo katika nyumba za ibada.

Ameongeza kuwa mbali na utoaji wa elimu hiyo mpaka sasa serikali imefanya jitihada za makusudi kuhakikisha wanatatua changamoto ya usafiri kupitia bajeti zinazotengwa kila mwaka pamoja na mikopo mbalimbali  ambayo inawasaidia kutatua tatizo hilo.

Ameongeza kuwa bado wanaendelea kukabiliana na changamoto hizo ambapo anaamini baada ya muda mfupi watakuwa wametatua changamoto hizo kwa kuongeza idadi ya magari na vizima moto vya kutoka kwa kila Mkoa.

Habari Kubwa