Jiji la Hamburg na Dar es Salaam kujadili mabadiliko tabia nchi

28Jun 2022
Mary Geofrey
DAR ES SALAAM
Nipashe
Jiji la Hamburg na Dar es Salaam kujadili mabadiliko tabia nchi

WADAU 30 kutoka katika Jiji la Hamburg nchini Ujerumani wanatarajia kuingia nchini Juni 30 mwaka huu, kwa ajili ya kujadili Mabadiliko ya Tabia Nchi wakati wa Maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki wa miji kati ya Jiji hilo na Dar es Salaam.

Wadau hao kutoka katika pande hizo mbili wanatoka katika taasisi mbalimbali za serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi na kupitia fursa hiyo wameona kuna umuhimu wa wao kukutana na kufanya majadiliano hayo ikiwa ni sehemu za juhudi za kushirikiana na serikali katika jitihada zake za jukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Urafiki kati ya majiji haya umechangia na kusaidia  kuboresha huduma katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya afya, mazingira, elimu, utafiti na utamaduni.

"Aidha, majiji haya yamewasaidia wataalamu wake na  wananchi kufanya ziara za kujifunza, kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi na utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

" Katika kipindi cha miaka 12 ya urafiki huu wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi na Jiji la Humburg wamekuwa mstari wa mbele katika uandaaji wa mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kufanya utafiti kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na namna ya kukabiliana nazo kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya mazingira," alisema

Urafiki wa jiji la Dar es Salaam na jiji la Humburg ulianza rasmi Julai Mosi, 2022 baada ya majiji hayo kutia saini hati ya makubaliano ya kuanzishwa kwa urafiki huo hivyo maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki wa majiji unatarajiwa kuwakutanisha wadau wengi kutoka katika sekta mbalimbali ambao watashauriana pia kuhusu njia bora ya kuimarisha urafiki huo na kuongeza idadi ya watu wanaonufaika na fursa zitokanazo na uhusiano huo.

Habari Kubwa