JK ashangazwa na Msukuma aliyefukuzwa Ikulu

30May 2020
Na Mwandishi Wetu
DODOMA
Nipashe
JK ashangazwa na Msukuma aliyefukuzwa Ikulu
  • "Lakini yule Msukuma sikukuambia umfukuze, lakini nilieleza tu masikitiko yangu"

Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ameshangwaza na maamuzi aliyoyachukua Rais Dk. John Pombe Magufuli, baada ya kumfukuza mfanyakazi mwenye kabila la Msukuma wa Ikulu, ambaye alishindwa kununua Mashine ya kutotoleshea mayai ya Tausi (Incubator).

Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Dk. Kikwete ameyasema hayo leo Mei 30, 2020, jijini Dodoma, wakati wa zoezi la kukabidhiwa ndege aina ya Tausi kwa Marais wastaafu pamoja na mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere pamoja na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa Ikulu Chamwino.

 Wakati akitoa salamu zake Rais Mstaafu Kikwete amesema "Mimi ndiyo mdogo nasema kwa niaba ya Wazee hawa, tunatoa shukrani kwa moyo wako wa upendo kwa kutupatia hawa ndege, tulikuwa tunawatamani lakini ukitoka nao, ukafika nao Msoga, watu watasema amepora, pia nakupongeza kwa maamuzi ya incubator lakini yule Msukuma sikukuambia umfukuze, lakini nilieleza tu masikitiko yangu" amesema Dk. Kikwete.

Wakati wa kutoa hobuta yake Rais Magufuli amesema "Wakati Rais Mstaafu Kikwete ananikabidihi Ikulu aliniambia ndege hawa wanataga mayai mengi, lakini huwa hawayalalii kuna mfanyakazi ni Msukuma mwenzio kila nikimuambia atafute Incubator itotoe mayai hafanyi, nilipoingia yule msukuma nikamfukuza kwanza" 

"Nataka niwahakikishie hawa ndege ni wenu, lakini nikajua kwamba inawezekana siku moja akaja mwingine akawanyang'anya nikaona nisaini kabisa kwamba nimewapa ni Nyara za Serikali lakini ninyi wanne mmeruhusiwa kuzitumia"

Aidha awali wakati akizungumza, Rais Magufuli amewapongeza Marais wote Wastaafu walioshiriki kuwatunza Tausi hao.

Habari Kubwa