Kikwete aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Makao makuu wa EAC jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa siku tano jukwaa la vijana la EAC linalofahamika Kama "YouLead" ulioandaliwa na Kituo cha Maendeleo, Uongozi na Utawala Bora cha MS TC DC na EAC.
Alisema vijana ni kundi kubwa linalofikia asilimia 80 ya watu wote wa Jumuiya, hivyo ni vyema wakashiriki kwa nguvu zote ili mawazo mengi yenye tija yaweze kuongeza chachu, lakini pia uimara wa mchakato wa kuifikisha EAC kwenye mtangamano kamili.
"Wasome mkataba una kila kitu, wajue kinachoendelea na kinachokusudiwa, sauti ya vijana ni muhimu katika ujenzi wa Jumuiya,” alieleza.
Mkurugenzi wa Programu wa MS TC DC, Sara Teri, alisema siku tano za mkutano watajadili ajenda za vijana kichumi kisiasa, kijamii na usalama, biashara zitakapomazilika Ijumaa wiki hii, vijana watakuwa na mkusanyiko na kuhitimisha maazimio kuhusiana na masuala waliyojadili.
Naye Mwenyekiti wa Bunge la zamani la vijana la EAC, Abdilahi Lugome, aliwataka vijana wa Tanzania kuchangamkia fursa zilizopo pamoja na kupigania kuanzishwa kwa Jukwa la Vijana Tanzania.
Alimuomba Rais John Magufuli kusadia kuanzishwa kwa baraza kwani sheria ambayo ilishatungwa imetamka juu ya kuanzishwa kwa Jukwaa hilo, ingawa utekelezaji bado.