JKT yawaita makambini wahitimu wengine kidato cha sita

10Jun 2021
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
JKT yawaita makambini wahitimu wengine kidato cha sita

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajab Mabele amewataka vijana wote walioitwa kuripoti makambini kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2021.

Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena.

Aidha Jeshi hilo limeongeza majina ya vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2021 kwenda kuungana na Vijana wenzao walioitwa hapo awali kuhudhuria mafunzo na kufanya idadi ya vijana walioitwa kwa mujibu wa sheria mwaka huu kufikia 40,000.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini hapa kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo,Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena amesema walitarajia kuwaita vijana 35,000 lakini waliotwa mpaka sasa jumla yao ni 40,000 huku akisistiza kuwa mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu tu.

"Naomba kusisitiza hapa,mafunzo ya vijana hawa kwa mwaka huu ni miezi mitatu tu na siyo mwaka mmoja kama ambavyo inasemekana hivi sasa,huko mitaani kuna watu wanasema mafunzo ni mwaka mmoja,hii siyo kweli" amesema Kanali Mabena.

Habari Kubwa