JKT yawaita waliorudishwa nyumbani

30Apr 2021
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe
JKT yawaita waliorudishwa nyumbani

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana kuripoti katika makambi ya JKT waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ya kujitolea kwa mwaka 2020/2021 waliorejeshwa majumbani Februali 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari Kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Charles Mbuge, Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT Kanali Hassan Mabena, amesema vijana wanaotakiwa kuripoti makambi ya JKT ni wale waliyokuwa wamepangiwa hapo awali ambao ni wa Elimu ya Darasa la Saba na Kidato cha Nne.

Kanali Mabena amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Mei saba hadi Mei 14, huku wale wenye elimu ya kidato cha sita, ngazi ya cheti,stashahada, shahada na wale wenye taaluma ya Uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi utaratibu mwingine utakapotangazwa.

Habari Kubwa