JPM aagiza kuzalisha chakula kusaidia waathirika Covid-19

18Jan 2021
Elizaberth Zaya
Dar es Salaam
Nipashe
JPM aagiza kuzalisha chakula kusaidia waathirika Covid-19

RAIS John Magufuli, amesisitiza umuhimu wa Watanzania kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula, ili kuyasaidia mataifa ambayo hakuna uzalishaji kutokana na wananchi wake kufungiwa ndani kuepuka kusambaa kwa maradhi ya Covid-19 katika nchi zao.

Rais aliyasema hayo jana alipoungana na waamini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Parokia ya Chato mkoani Geita kusali Misa Takatifu iliyoongozwa na Paroko, Padre Henry Mulinganisa.

Alisema Mungu ameiepusha Tanzania na corona, hivyo Watanzania wanapaswa kuitumia nafasi hiyo kuchapa kazi zaidi hasa kuzalisha mazao mbalimbali yakiwamo ya chakula kwa ajili ya kuzisaidia nchi ambazo zinashindwa kufanya uzalishaji kutokana na watu wake kufungiwa majumbani na pia kukuza uchumi.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa