Jumuiya ya watumia maji Mgeta A yakabidhiwa mashine kufyatulia tofali

12Aug 2020
Na Mwandishi Wetu
MOROGORO
Nipashe
Jumuiya ya watumia maji Mgeta A yakabidhiwa mashine kufyatulia tofali

Bodi ya Maji Bonde la Mto Wami/Ruvu imetoa mashine ya kufyatulia matofali ya 'Interlock' kwa Jumuiya ya watumia maji ya Mgeta Juu A mkoani Morogoro ili kujiongezea kipato na kuwawezesha katika utunzaji na uhifadhi wa Rasilimali za maji.

Wanajumuiya ya mgeta juu a wakifyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi yao baada ya kupewa mafunzo jinsi ya kuitumia mashine hiyo.

Bodi ya Maji Bonde la Mto Wami/Ruvu imetoa mashine za kufyatulia matofali ya Interlock kwa Jumuiya ya watumia maji ya Mgeta Juu A mkoani Morogoro.

Mashine hiyo zimetolewa kupitia mradi wa uendelezaji wa sekta ya maji awamu ya pili (Water Sector Supporting project WSSP 11) na kupitia mashine hiyo itawawezesha wanajumuiya hao kufyatua tofali za kujenga Ofisi yao pamoja na kuwa chanzo cha mapato kitakachowawezesha kupata fedha kwa ajili ya kujiendesha na usimamizi wa Rasilimali za Maji katika eneo hilo.

Mwalimu akikagua tofali zilizotengenezwa na wanajumuiya ya Mgeta juu A baada ya kupata mafunzo.
Baadhi ya matofali yaliyokwisha kufyatuliwa na wana Jumuiya wa Mgeta juu A.

Miti rafiki na maji inayotarajiwa kupandwa pembezoni mwa mto mgeta.

Washiriki wakifundishwa jinsi ya kupata miti hiyo kitaalamu.
Mtaalamu wa misitu kutoka ofisi ya TFS akiwafundisha jumuiya ya Mgeta juu A jinsi ya kutengeneza kiriba cha kisia mbegu za miti rafiki na maji.

Habari Kubwa