Jumuiya za maji kupunguza gharama za maji,kuunganisha kwa mkopo

13Apr 2019
Frank Monyo
Dar es salaam
Nipashe
Jumuiya za maji kupunguza gharama za maji,kuunganisha kwa mkopo

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja ameagiza Jumuiya za watumia maji Dar es salaam kupunguza gharama za maji na kuwauzia wananchi kwa bei elekezi 1,663 kwa mwezi.

Mkuu wa Kitengo Cha uhusiano kwa umma dawasa, neli msuya (kulia) akimuelekeza afisa mtendaji mkuu wa dawasa mhandisi cyprian luhemeja ramani ya usambazaji wa Maji katika mradi wa jumuiya za watumia maji.

Aidha amezitaka Jumuiya hizo kuwaunganisha wateja wanaohitaji huduma hiyo kwa mkopo utakaolipwa ndani ya miezi sita au mwaka.

Hayo amezungumza leo wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya Jumuiya ya watumia Maji wa Domu katika Kata ya Makangarawe.

Pia ameagiza kupitiwa upya gharama za maji ili ziweze kupunguzwa na kufikia bei elekezi 1,663 kwa ujazo wa lita 1,000 ili kuwa na uwiano sawa wa bei za maji kwa wateja wote.

Amesema moja kati ya kazi za DAWASA ni kuhakikisha watu wanapata huduma ya maji "Haina maana maji yatoke Ruvujuu au Ruvuchini au dhana ya watu kusema maji haya  ya Jumuiya za watumia Maji sio ya DAWASA hizi Jumuiya zote zipo chini yetu." Amesema Mhandisi Luhemeja

Amesema angependa kuona wananchi wengi wanahudumiwa na jumuiya hizo na kuagiza wasinamizi wa Jumuiya hiyo kuendelea na mchakato wa kuwaunganishia maji kwa njia ya mkopo wananchi  na kufanya malipo kwa miezi sita hadi 12.

Shukrani za Afisa Mtendaji Mkuu Dawasa Mhandisi Luhemeja kwa wasimamizi wa miradi anaosaidia kutoa huduma ya maji pembezoni.

Habari Kubwa