Kalemani aagiza kukamatwa kwa Mkandarasi wa Njarite

30Jul 2021
Mary Mosha
Same
Nipashe
Kalemani aagiza kukamatwa kwa Mkandarasi wa Njarite

​​​​​​​WAZIRI wa Nishati, Dk. Medadi Kalemani, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kumsaka na kumkamata Mkandarasi wa Kampuni ya Njarite kutokana na kushindwa kutekeleza kazi ya kuwaunganishia Wananchi umeme kwa  kutokuwepo kwenye eneo lake la kazi  huku akitoa miezi miwili-

​​​​​​​WAZIRI wa Nishati, Dk. Medadi Kalemani.

-kwa  Kampuni za  ukandarasi ya Ubarn & Rural Engineering Services na kampuni ya Octopus Enginearing kukamilisha ufungaji wa umeme kwa vijiji 10  zilivyobakia.

Akizungumza leo katika uzinduzi wa  wa mradi wa ujazilizi (Densification Project) uliofanyika katika  shule ya msingi Kalemani iliyopo kkatika Kata ya Maore, tarafa ya Ndungu  jimbo la Same Mashariki.

“Mkuu wa Wilaya  ya Same hakikisha Mkandarasi huyu anasakwa na kutiwa mbaroni kwa mahojiano ya kina, wapo baadhi yao wanafanya kazi kwa miaka sita sasa tangu REA awamu ya pili, wameweka nguzo na kutokomea kusikojulika huku wananchi wakiendelea kuteseka, tukiwaita kwenye mikutano kama hii hawafiki, na tayari tumewalipa fedha za serikali,”

“Serikali imetenga zaidi ya bilioni 27.2 kwa  mkoa wa Kilimanjaro , mnawakandarasi wengi   ambao jukumu lao ni kusambaza umeme sitegemei kusikia wananchi wakilalamika ukosekanaji wa umeme, nimekuja  na timu ya wataalamu wangu kutatua kero za wananchi na si kuhubiri na kutoa siasa, umeme ni 27,000 tu hatutaki ukiritimba wa kuwaunganishia umeme kwa 700,000 hadi 1,000,000, kwa mtaalamu atakayekaidi agizo hilo hatoshi kwenye nafasi yake” amesema Waziri Kalemani.

Aidha, Waziri huyo ametoa mwezi moja kwa Shirika la  Umeme nchini (TANESCO) kuujenga kituo cha kupoozea umeme katika tarafa ya Gonja na kuweka ofisi ndogo kwa lengo la kuwahudumia Wananchi wa Kanda ya Milimani wilayani humo.

“Nimesikia kwenye risala, tatizo la kukatika kwa umeme na kurudi baada ya siku mbili linapelekea huduma muhimu katika Hospitali ya Gonja kukwama hili ni jambo hatari  na lazima lichukuliwe hatua za haraka, nimeagiza kituo  kikamilike ifikapo septemba 1 mwaka huu na wapelekwe wataalamu watakaosaidia utapikanaji wa huduma za umeme kwa wananchi na taasisi,” amesema Waziri.

“Katika wilaya Same Vipo 10  kati ya 100 ambavyo hazijaunganishiwa umeme na kampuni ya  Ubarn & Rural Engineering Services inavijiji  23 ambapo bado hawajakamilisha vijiji nane, na  kampuni yaOctopus Enginearing inavijiji 27 haijakamilisha  vijiji vitano tu,”amesema Meneja Jaston Bayasabe.    

Akisoma risala Ofisa Tarafa wa Gonja Ibrahimu Malisa, “Wanachi wa tarafa ya gonja wanaomba  kufikishiwa umeme katika Vitongoji  Miyoye,Putu, Mjema Kati, Chamakindi Ngwero, Mgongo, Mahande , Mtii Riane Mdariani Ngara Kibutu Mareti, Chati MwalaVunje,”

Habari Kubwa