Kama unajua ndugu yako ni jambazi nenda Muhimbili –SACP Mambosasa

25May 2020
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Kama unajua ndugu yako ni jambazi nenda Muhimbili –SACP Mambosasa

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amewataka watu ambao wanajua kuwa ndugu zao ni majambazi na wanajua kabisa walienda kutafuta lakini hawajarudi, basi waende Muhimbili kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao.

SACP Lazaro Mambosasa.

SACP Mambosasa amesema hayo leo wakati akitoa taarifa za kuuawa kwa majambazi saba wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi usiku wa kuamkia leo, walipokuwa wakienda kufanya tukio katika ghala la GS Group Limited.

Hayo ameyabainisha leo Mei 25, 2020, wakati akitoa taarifa za majambazi saba waliouawa wakati wa majibizano ya risasi na Polisi usiku wa kuamkia leo, waliokuwa wakielekea kufanya ujambazi katika ghala la GS Group Limited, ambapo kwa bahati mbaya majambazi hao majina yao hayakuweza kufahamika.

"Kama unavyoelewa hakukuwa na mahojiano kati ya Jeshi la Polisi na wahusika, walipoona wanafuatiliwa walianza kukimbia, walianza kusalimia kwa kurusha risasi na Askari wakajibu, mpaka sasa sina majina ya wahusika lakini mtu yeyote anaweza kwenda Muhimbili kwa ajili ya kutafuta kama anajua, kuna ndugu yake jambazi haonekani alienda kuvuna ameshindwa kurudi, basi aende Muhimbili ataweza kumtambua ndugu yake" amesema Kamanda Mambosasa

Habari Kubwa