Kamanda Shana afariki dunia

16Sep 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kamanda Shana afariki dunia

Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha amethibitisha hilo leo Septemba 16, 2020 na kusema kuwa marehemu alikaa hospitalini hapo kwa siku 21 na kati ya hizo alikaa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), kwa siku tatu.

"Jonathan Shana, Mstaafu RPC Mkoa wa Arusha amefariki usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, amelazwa hapa Muhimbili kwa siku 21, na kati ya siku hizo ICU amekaa siku 3", amesema Aligaesha.

Juni 24,2020, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha ACP Shana kutoka kuwa RPC na kwenda kuwa afisa mnadhimu shule ya Polisi Moshi.

Habari Kubwa