Kamati ya amani Shinyanga yakemea vurugu uchaguzi mkuu

20Oct 2020
Marco Maduhu
Shinyanga.
Nipashe
Kamati ya amani Shinyanga yakemea vurugu uchaguzi mkuu

Kamati ya amani mkoani Shinyanga imewataka Watanzania kutokubali kutumiwa na wanasiasa siku ya kupiga kura kufanya fujo ambazo zitavuruga amani ya nchi.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya amani mkoani Shinyanga Sheikh Khalfan Ally, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakati wa kutoa tamko kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Sheikh Khalfan Ally, amebainisha hayo leo wakati akisoma tamko la viongozi wa dini mkoani humo, kutokana na kuwepo viashiria kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, kuanza kuhamasisha  wananchi kufanya fujo siku hiyo ya uchaguzi Oktoba 28,2020.

Amesema Watanzania wanapaswa kuilinda amani ya nchi ambayo inatamaniwa na baadhi ya mataifa kuona ikivurugika, bali wakatae kushawishiwa na baadhi ya wanasiasa kufanya fujo kwenye uchaguzi mkuu, ili kupeuka uvunjifu huo wa amani.

“Kamati ya amani mkoani Shinyanga inawataka Watanzania kutokubali kutumiwa  na wanasiasa kuvuruga amani ya nchi kwenye uchaguzi mkuu, bali siku hiyo wakimaliza kupiga kura warudi majumbani mwao kusubili matokeo na wasifanye maandamano ya aina yoyote ile,” aamesema Sheikh  Ally na kuongeza kuwa;

“Uvunjifu wa amani ukitokea waathirika wakubwa ni watoto, akina mama, wazee na watu wenye mahitaji maalum, pamoja na uchumi wa nchi kuyumba, sababu hapatakuwa na shughuli zozote zile za maendeleo,” amesema 

Wajumbe na viongozi wa kamati ya amani Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Habari Kubwa