Kamati ya Bunge Bajeti yaipa kongole MSD

14Oct 2021
Mary Geofrey
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kamati ya Bunge Bajeti yaipa kongole MSD

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  Daniel Sillo, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa jitihada kubwa inazozizifanya kuboreshaji upatikanaji wa bidhaa za afya nchini kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na kuboresha viwanda vya dawa vilivyokuwa na hali mbaya.

Sillo ametoa pongezi hizo leo, wakati kamati hiyo ilipokuwa ziarani MSD, ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa kamati hiyo walitembelea kiwanda cha dawa cha Keko, Kiwanda cha MSD cha kuzalisha Barakoa pamoja na maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya dawa yaliyopo Keko. 

Amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Meja Jenerali Gabriel Mhidze, na Watendaji wote wa MSD kwa maono yao ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba kwa sababu ununuzi wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi na kwingineko umekuwa ukiigharimu serikali fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kuboresha huduma nyingine.

“Kamati yetu imesikia changamoto kutoka kwenu zinazowakwamisha kusonga mbele, tunazichukua na kuzifikisha serikalini ili kuhakikisha MSD inaimarika ipasavyo ili kuwezesha upatikanaji wa dawa nchini". 

Naye Mkurugenzi Mkuu  wa MSD, Meja Jenerali Mhidze, ameeleza kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili MSD bado inaendelea kutoa huduma bora na za kiwango cha juu kwa wananchi na kusimamia mnyororo wa ugavi, ili kuleta tija kwenye mfumo wa afya wa nchi.

Habari Kubwa