Kamati ya Ulinzi na Usalama Dodoma kuimarisha usalama Mkutano Mkuu CCM

07Jul 2020
Dotto Lameck
Dodoma
Nipashe
Kamati ya Ulinzi na Usalama Dodoma kuimarisha usalama Mkutano Mkuu CCM

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma (SAC), Gilles Muroto, amesema Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama wamejipanga kudhibiti vitendo vya kitapeli kwa wanaojifanya wapo karibu na viongozi wakuu wa Kitaifa wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi-

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (SAC), Gilles Muroto.

-wa Uchaguzi wa CCM utakaoanza leo na kumalizika Julai 12, Mwaka huu .

“Jeshi limejipanga kuhakikisha yeyote atakayejaribu kufanya utapeli wa kujifanya wapo karibu na viongozi wakuu wa kitaifa hawataondoka Dodoma wajipange kubakia na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria,” amesema Kamanda Muroto.

Muroto amesema mkutano huo unatarajiwa kuwa na wajumbe zaidi ya 3,000 hivyo hawatapenda kuwaona watu wanaotaka kutenda vitendo vya kitapeli kwa kujifanya wapo karibu na viongozi hao.

Aidha, Kamanda huyo amesema uzoefu unaonesha kuwa katika mikutano kama hiyo wamekuwa wakihudhuria watu mbalimbali wakiwemo wapambe wa wagombea, familia za wagombea, wapiga debe, wajasiliamali lakini pia wanakuwepo watu wabaya ambao wanatumia fursa hiyo kutekeleza azma yao ya kihalifu.

Hata hivyo, Muroto ametoa onyo kwa makundi hayo ambayo yanapanga kufanya vitendo vya kihalifu wasije wakaingia katika mtego ambao hawakutarajia kwa kuwa jeshi hilo limejiandaa kikamilifu kulinda amani ya wananchi.

Habari Kubwa