Kamati za Bunge kukutana Jan. 18

14Jan 2021
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Kamati za Bunge kukutana Jan. 18

KAMATI za Kudumu za Bunge la 12, zinatarajiwa kuanza vikao vyake wiki ijayo huku miongoni mwa shughuli zitakazofanyika ni pamoja na uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, kamati hizo zitakutana kutekeleza majukumu ya kibunge kuanzia Januari 18 hadi 31, mwaka huu, kabla ya kuanza mkutano wa pili wa Bunge Februari 2, mwaka huu.

Ilieleza kuwa kamati hizo zitaanza kwa kufanya uchaguzi wa wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati zote.

Pia kwa muda huo kutakuwapo na mafunzo kwenye kamati mbalimbali ikiwamo ya majukumu na taratibu za uendeshaji wa kila kamati.

Mafunzo mengine ni kuhusu Bunge mtandao na usalama wa mtandao kwa kamati zote, kamati za kisekta kupokea maelekezo ya wizara kuhusu muundo, majukumu ya taasisi pamoja na sera na sheria zinazosimamiwa na wizara hizo.

Soma zaidi; https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa