Kampeni ya utoaji chanjo ya Uviko-19 yaanza Mwanza

17Sep 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Kampeni ya utoaji chanjo ya Uviko-19 yaanza Mwanza

MKOA wa Mwanza umeanza kampeni ya utoaji chanjo ya UVIKO-19 katika maeneo yote hasa maeneo yasiyofikaka ili jamii iwe salama na kuleta maendeleo na kukuza  uchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel.

Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel. Amesema kuwa kuna dalili nzuri kwa wananchi kuanza kuelewa kuhusu chanjo hiyo ni baada ya kupata elimu.

Amesema idadi ya waliopata chanjo ni kubwa hivyo amewataka wananchi kujitokeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo kata ya Buhongwa,Mkuyuni,butimba  kupata chanjo ili kuhakikisha wapo salama .

Aidha amewataka wataalamu wa afya mkoa kupanua wigo ili kuifikia jamii yote kwa uharaka na kuendelea kuhamasisha jamii kuhusiana na chanjo.

" Chanjo ni hiari lakini kuna baadhi ya mambo uwezi kuyafanya bila kuchanja hakuna Taifa lisilopenda raia wake mimi nilipiga chanjo kidogo nimepata ujasiri nikikooa kidogo sina hofu kabisa najua nipo salama " ameeleza Gabriel.