Kampuni ya Bwiru yatoa seti 20 vifaa maalum kijikinga corona

28May 2020
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Kampuni ya Bwiru yatoa seti 20 vifaa maalum kijikinga corona

Kampuni ya Bwiru Intertaiment watoa seti 20 za vifaa vya kuvaa watoa huduma wa afya vyenye thamani ya milion moja ili kuwakinga na maambukizi wakati wakitoa huduma kwa waathirika wa ugonjwa corona.

Akizungumza wakati akitoa msaada huo leo jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Grace Todd, amesema wamenunua vifaa hivyo vinavyotengenezwa katika Hosptali ya Taifa Muhimbili ili kuwapatia madaktari ili kuwanusuru madaktari wanapokuwa wakitoa huduma ili wasipate maambukuzo.

"Tunaungana na ofisi ya mkuu wa mkoa ili kukabiliana na ugonjwa huo ambapo vifaa hivi tulivyotoa ni mchango wetu mdogo na tulivyoona ni muhimu lakini imani yetu vitasaidia kuwakinga ,kuwaweka salama madaktari wetu dhidi ya gonjwa hili" amesema Todd.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewashukuru kwa kuonyesha uzalendo mkubwa kwa kununua bidhaa zilizozalishwa nchini hivyo aliwataka wadau mbalimbali wajitokeze na kuunganisha nguvu katika mapambano ya kujikinga na kuwakinga wengine na corona.

"Hizi bidhaa zimezalishwa nchini sasa watanzania tunaweza kufanya vitu ambavyo zamani tulishindwa na tulikuwa tunakimbilia kununua nje "amesema Mongella

Habari Kubwa