Kandege aipongeza Kinondoni ujenzi uwanja wa kisasa

25Jun 2020
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Kandege aipongeza Kinondoni ujenzi uwanja wa kisasa

NAIBU wa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Josephat Kandege, ameipongeza Manispaa ya Manispaa ya Kinondoni kwa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 3600 kwa mara moja.

Kandege ametoa pongezi hizo alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Halmashauri hiyo ya kushuhudia ujenzi wa uwanja huo wa kisasa unaoendelea kujengwa ambao unakadiriwa kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 2.2.

Aidha, Kandege amesema mradi huo ukikamilika utaiwezesha timu ya mpira ya Manispaa hiyo ya KMC Fc kupata faida kubwa na pia itaweza kujiendesha yenyewe kupitia mapato yatakayokusanywa katika uwanja huo, huku akizitaka timu kubwa ambazo hazina viwanja hadi sasa kuiga mfano huo.

“Niwapongeze sana Kinondoni, kwakujenga uwanja huu, utakapomalizika najua faida yake ipo wazi kabisa, kwanza inapendezesha, lakini pia inaleta changamoto kwa Halmashauri nyingine na timu kubwa kuiga kwenu, kama timu ya Kinondoni inaweza kuwa na uwanja wa kisasa wao wanashindwa nini” amesema Mhe. Kandege.

Habari Kubwa