Kanisa lakanusha wanawake waliozaa

26Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kanisa lakanusha wanawake waliozaa

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limekanusha kupiga marufuku ufungishaji ndoa madhabahuni kwa wanawake waliozaa.

Barua ya juzi ya Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Godfrey Nkini, iliyoifikia Nipashe jana ilisema hakuna waraka au tangazo lolote la kanisa hilo ambalo liliwahi kutolewa kuhusu suala hilo.

Toleo la mwishoni la Nipashe Jumapili liliandika kuwa KKKT imepiga marufuku ufungishaji ndoa madhabahuni kwa wanawake waliozaa.

Aidha, habari hiyo ambayo chanzo chake kilikuwa tangazo lililodaiwa kutolewa katika Mtaa wa Neema, ilidai KKKT imepiga marufuku pia wanawake wenye ujauzito kufunga ndoa madhahabuni kwa maelezo kuwa kufanya hivyo ni kukiuka maandiko ya Mungu.

Lakini taarifa ya Nkini ilisema: "Habari iliyohusisha Mtaa wa Neema, ni ya uongo na imepotosha umma.

Taarifa hiyo pia ilisema hapakuwa na tangazo lolote lililotolewa na KKKT kama ilivyoandikwa.

Alipoulizwa ufafanuzi juu ya tangazo hilo wakati wa ufuatiliaji wiki iliyopita, Mkuu wa Jimbo la Kaskazini, mchungaji Anta Muro hakukubali wala kukataa kutangazwa kwake badala yake alimwomba mwandishi kuwasiliana na gazeti la Upendo linalomilikiwa na kanisa hilo.

Chanzo kimoja ya chabari kiliimbia Nipashe Jumapili kuwa tangazo hilo lilitolewa ibadani katika Mtaa wa Neema, Usharika wa Mbezi Luis wiki mbili zilizopita.

Habari Kubwa