Kanyasu aonya wanaojenga kiholela ushoroba

25May 2020
Dotto Lameck
Babati
Nipashe
Kanyasu aonya wanaojenga kiholela ushoroba

​​​​​​​NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, amesema kuwa serikali itachukua hatua kwa watu wanaokaidi amri ya kutojenga na kutofanya shughuli za kibinadamu kwenye mapito ya wanyamapori (ushoroba) kwa kuwa wanachangia kufifisha juhudi za wadau wa uhifadhi na kusababisha-

-mogogoro inayoendelea kati ya binadamu na wanyamapori.

Kanyasu amesema kwa watu wanaojenga nyumba kiholela katika maeneo ya Ushoroba hawatalipwa fidia na badala yake watachukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Maurusi Msuha amesema uainishwaji, upimaji, na uwekaji wa mipaka ya maeneo ya ushoroba unapaswa kushirikisha wananchi ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima

Naye Katibu wa Jumuiya ya hifadhi ya Jamii, Burunge, Benson Mwaise pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu wamesema elimu kwa wananchi inahitajika ili kufanikiwa kulinda ushoroba.

Habari Kubwa