Katambi kutatua changamoto uzio Zahanati ya Oldshinyanga

20Jul 2021
Marco Maduhu
SHINYANGA
Nipashe
Katambi kutatua changamoto uzio Zahanati ya Oldshinyanga

Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ameahidi kutatua changamoto ya ukosefu wa uzio katika Zahanati ya Oldshinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, amebainisha hayo leo kwenye mkutano wa hadhara Oldshinyanga.

Amesema amesikia kilio cha akina mama kwenye kata hiyo, ambacho atakifanyia kazi, ili waendelee kupata huduma bora ya afya, pamoja na kuongeza watumishi na madawa, kwenye zahanati hiyo.

"Katika Bajeti ya mwaka wa fedha (2021/2022) kuna Sh.biloni 45 ambazo zitajenga maboma nchi nzima, na bilioni 31,2 kujenga Zahanati 500, hivyo uzio wa kwenye Zahanati hii utajengwa tu mama zangu," amesema Katambi.

Diwani wa Viti Maalum Picca Chogelo, akiwasilisha kero ya akina mama ya ukosefu wa uzio na Jengo la kujifungua akina mama katika Zahanati ya Oldshinyanga, kwenye mkutano wa Mbunge Katambi.

Katika hatua nyingine Katambi, ameahidi kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi kwenye zahanati hiyo na ununuzi wa madawa.

Awali akiwasilisha kilio kwa niaba ya akina mama juu ya ukosefu wa uzio kwenye Zahanati ya Oldshinyanga, Diwani wa Vitimaalum Picca Chogelo, amesema wanawake wanaofika kujifungua wanapata shida wakati wa mazoezi, ambapo hukumbana na mifugo na kuhatarisha maisha yao.

Mbali na kuomba kujengewa uzio, pia wameomba kujengewa Jengo la mama na mtoto kwa ajili ya kujifungua, ambapo kwenye zahanati hiyo halipo.

Habari Kubwa