Katibu UWT aunga mkono kauli ya Rais Magufuli

22Feb 2021
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Katibu UWT aunga mkono kauli ya Rais Magufuli

KATIBU wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa, ameunga mkono kauli ya Rais Dk John Magufuli ya kuhimiza Watanzania kufanya maombi huku akisema kuwa huo ni uthibitisho wa jinsi gani Tanzania ina kiongozi mwenye maono na mwenye hofu ya Mungu.

Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa.

Madukwa amesema katika kipindi hiki ambacho Watanzania wengi wamekua na hofu inayosababishwa na kutishwa na baadhi ya watu wasio na mapenzi mema juu ya ugonjwa wa kushindwa kupumua, Rais Dk Magufuli ametoa kauli iliyozalisha tumaini jipya kwa watanzania walio wengi.

Aidha, Madukwa amesema hata mwaka jana wakati ugonjwa huo ukishika kasi sehemu mbalimbali duniani, Dk Magufuli alisimama na kuwataka Watanzania kila mmoja kwa imani yake kumuomba Mungu jambo ambalo lilisaidia kuondoa ugonjwa huo na kusaidia Tanzania kuendelea na shughuli zake za kiuchumi bila Rais kufungia watu ndani kama Nchi zingine zilivyokua zikifanya. 

"Ni haya haya maombi ambayo Rais Dk Magufuli amesema tuyafanye ndio alituhimiza mwaka jana tuyafanye na tukaushinda ugonjwa huu kiasi kwamba tukawa tunaendelea na shughuli zetu bila kufungiwa ndani na uchumi wetu ukapaa hadi kufikia uchumi wa kati, hivyo naungana na Rais wetu mpendwa ya kwamba maombi ndio njia pekee ya kuishinda hofu tuliyonayo kuhusiana na ugonjwa wa corona,”amesema Madukwa.