Katibu Mkuu afya awapumzisha wajumbe nane

19May 2019
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe Jumapili
Katibu Mkuu afya awapumzisha wajumbe nane

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya katika ofisi ya Rais Tamisemi, amewapumzisha majukumu ya uongozi wajumbe nane wa timu ya uendeshaji na usimamizi huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida-

kwa kushindwa kuwajibika kikamilifu katika kutekeleza wajibu wao wa msingi. Hivyo, amewataka waendelee na majukumu yao ya kitaaluma kwa mujibu wa ajira zao badala ya majukumu ya uongozi hadi hapo itakapoelekezwa vinginevyo.

Ameyasema hayo wakati akikagua utendaji kazi wa watoa huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida

Dkt. Gwajima amemuagiza mganga mkuu wa mkoa wa singida Dkt Victorina Ludovick kushirikiana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuteua timu ya mpito hadi hapo uchambuzi wa kina cha uzembe utakapofanyika kwa ajili ya hatua zaidi.

Ameagiza timu iliyopumzishwa majukumu ya uongozi kutoa maelezo ndani ya siku 7 kwanini walishindwa kusimamia kikamilifu utendaji kazi wa kituo hicho na kwa nini wasivuliwe majukumu ya uongozi jumla.

Vilevile, amemtaka mganga mkuu wa mkoa wa singida na timu yake nao kutoa maelezo kwa nini wameshindwa kubaini uzembe wa uwajibikaji wa timu ya usimamizi na uendeshaji huduma halmashauri ya wilaya hiyo na kwa nini nao wasiwe sehemu ya kuchangia tatizo.

Dkt. Gwajima ameitaka timu ya afya Mkoa kutoondoka Manyoni hadi changamoto zote zinazohitaji hatua za haraka zifanyiwe kazi na atoe taarifa Ofisi ya Rais Tamisemi ambayo itarejea kwa ukaguzi wa kina.

Aidha, Dkt Gwajima amewapongeza watoa huduma walioko mawodini kwa kujituma katika kuhudumia wagonjwa.

Habari Kubwa