Katibu Mkuu Dk.Michael ataja mikakati yake

20Jun 2022
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Katibu Mkuu Dk.Michael ataja mikakati yake

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.Francis Michael ametaja mikakati mbalimbali atakayoisimamia kwenye elimu ikiwamo kuimarisha vyuo vya kati ili kukidhi mahitaji ya wataalamu yaliyopo.

Dk Michael ameyasema hayo leo jijini hapa mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema atatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia mipango na mikakati ya wizara, maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ikiwamo mapitio ya mitaala.

Katibu huyo amesema atawasiliana na Ofisi ya Rais, Utumishi ili kujua maeneo yenye uhitaji mkubwa wa watumishi ili mabadiliko ya mitaala yazingatie eneo hilo ili kuwa na wataalam wanaokidhi mahitaji ya serikali.

Habari Kubwa