Katibu mwenezi Chadema asimamishwa kwa usaliti 

21Jan 2020
Marco Maduhu
Shinyanga.
Nipashe
Katibu mwenezi Chadema asimamishwa kwa usaliti 

CHAMA cha Chadema mkoani Shinyanga, kimemsimamisha Katibu Mwenezi wa chama hicho Charles Shigino, kutoendelea tena na nafasi hiyo kwa madai ya kukiuka katiba ya chama, na kuonyesha utovu wa nidhamu, mara baada ya kuandika barua Polisi kuzuia mkutano wa Chama-

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi, akizungumza na waandishi wa habari, juu ya maamuzi ya baraza la uongozi mkoa ambapo limearidhia kumsimamisha ukatibu mwenezi wa jimbo la Shinyanga Charles Shigino kulia ni Katibu wa Chadema mkoa wa Shinyanga Zacharia Obad.

- akidai hautambui na una hatarisha hali ya usalama.

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi akizungumza na Wana- Chadema kwenye Ofisi za Chadema wilaya ya Shinyanga mara baada ya mkutano wao kuzuiwa na Jeshi la Polisi kutokana na Katibu wao Mwenezi Jimbo la Shinyanga Charles Shigino kupeleka barua Polisi ya kutoufahamu mkutano huo na una hatarisha hali ya kiusalama.-hicho akidai hautambui na una hatarisha hali ya usalama.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi, amesema leo ilikuwa wafanye mkutano wa Chama pamoja na kupeana maelekezo ya chama kutoka ngazi za juu, sambamba na kukijenga chama katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika Oktoba mwaka huu.

Amesema wakati akijiandaa na mkutano, walikuta Askali Polisi wakiwa wametanda kwenye eneo ambalo walipanga kufanya mkutano huo kwenye Hoteli ya Ibanza iliyopo Kata ya Ibinzamata Shinyanga mjini, waka ambiwa hawawezi kufanya mkutano huo kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazotishia hali ya kiusalama.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akizungumza na Wanachama wa Chadema kwenye Ofisi za Chadema Wilaya ya Shinyanga mara baada ya mkutano wao kuzuiwa na Jeshi la Polisi kutokana na Katibu wao Mwenezi Jimbo la Shinyanga Charles Shigino kupeleka barua Polisi ya kutoufahamu mkutano huo na una hatarisha hali ya kiusalama.

“Chama cha demokrasia na maendeleo chadema leo tulikuwa na mkutano ambao ulikuwa na ajenda mbalimbali za kujadili, na kupeana maelekezo ya chama kutoka ngazi za juu, pamoja na kukijenga chama katika kuelekea kwenye kipidi cha uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwaka Oktoba mwaka huu,” amesema Ntobi na kuongeza;

“Wakati tukijiandaa na mkutano huo ndipo Jeshi la Polisi likatuzuia kutofanya mkutano, na tulipohoji ni kwanini, tukaambiwa kuwa katibu mwenezi wetu Charles Shigino ameandika barua Polisi ya kutoutambua mkutano na una hatarisha hali ya usalama, ndipo kuamua kuuhairisha mkutano huu hadi siku nyingine,”

Wanachama wa CHADEMA wakiwa kwenye Ofisi zao iliyopo Wilaya ya Shinyanga, mara baada ya mkutano wao kuzuia wa Jeshi la Polisi ambao ulikuwa ufanyike kwenye Hoteli ya Ibanza Shinyanga mjini.

Aidha amesema kutokana na katibu mwenezi huyo kukeuka katiba ya Chama na kuonyesha utovu wa nidhamu na kukisaliti Chama, baraza la uongozi la mkoa limeadhimia kumsimamisha nafasi yake ya uenezi jimbo la Shinyanga, pamoja na ujumbe wa mkutano mkuu Kata ya Ngokolo.

Naye Katibu Mwenezi wa Chama hicho, Chalres Shigino, amekiri kuandika barua kwa Jeshi hilo la kuzuia mkutano huo, kwa madai ni batili na umekeuka katiba ya chama, akidai hakupewa taarifa juu ya kuwapo kwa mkutano huo, ambapo yeye ndiye mratibu wa mikutano yote ndipo akaamua kuuzuia.

Pia amesema yeye bado ni Katibu Mwenezi wa Chadema Jimbo la Shinyanga kwa sababu taratibu za kumvua uongozi huo hazijafuatwa.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Deborah Magiligimba, alikiri kuuzuia mkutano huo wa Chadema, mara baada ya kutokea Sinto fahamu kati yao nakubainisha jambo ambalo ni hatari kiusalama, ambapo aliwa amuru wakaelewane kwanza ndipo waruhusiwe kufanya mkutano huo tena.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Charles Shigino, akizungumza na vyombo vya habari akikiri kupeleka barua hiyo kwa Jeshi la Polisi akidai mkutano huo hautambui ni batili.

Habari Kubwa