Katibu UVCCM auawa kwa kunyongwa

18Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Katibu UVCCM auawa kwa kunyongwa

Jeshi la polisi mkoani Kagera limeanza uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Kata ya Katoke wilayani Muleba.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi.

Mwili wa Jaspar Jasson mwenye umri wa miaka 41, umekutwa kando kando ya barabara Asubuhi ya jana, Februari 17 huku ukiwa na michubuko ya kamba shingoni.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mwili huo umekutwa na dalili zote za kunyongwa au kujinyonga lakini kinacholeta utata ni eneo ulipokutwa, kwakuwa hakuna mti wala alama zinazoonyesha kuwa tukio limetokea katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa kamanda Malimi, baba huyo alionekana hadharani kwa mara ya mwisho Februari 16, Saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Bisore alikohamia baada ya kutelekeza familia yake na kwenda kuishi na mwanamke mwingine na kwamba upelelezi kuhusiana na tukio hilo umeanza, huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Chanzo: Eatv

Habari Kubwa