Kauli ya Makonda baada ya Magufuli kumtaka arejeshe pesa za Tasaf

17Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR
Nipashe
Kauli ya Makonda baada ya Magufuli kumtaka arejeshe pesa za Tasaf

Baada ya Rais Dkt John Magufuli kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuzirudisha zile pesa za TASAF alizodai kupewa na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa mwaka 2012.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkuu huyo wa mkoa ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagramu kuandika kuwa "Wakati tunasambaza hizi habari za TASAF kwa kasi kubwa huku tukifurahia jina la MAKONDA kutajwa, Naomba kwa kasi hiyo hiyo tusambaze habari za Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Tume yetu ya Uchaguzi. Kwani muda siyo rafiki huku tukifurahia majina yetu kuwepo kwenye vitabu vya NEC".

Leo Februari 17, 2020, wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF, Rais Magufuli wakati wa hotuba yake alizitaja changamoto zilizojitokeza katika zoezi la uhakiki wa Kaya maskini, lililofanyika 2015 hadi June 2017, ambapo zilibainika kaya hewa 73,561.

"Kaya 22,034 zilithibitika wanakaya wake siyo maskini na mojawapo ni akina Makonda ambao walizitumia fedha hizo kwenda Dodoma wakati siyo maskini na ninaomba kama hili ni ukweli Makonda azirudishe hizo fedha, kama kweli alituma fedha za TASAF lazima hizo fedha azirudishe" amesema Rais Magufuli.

Katika hotuba yake Makonda alieleza ni kwa namna gani Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, alivyompatia fedha za TASAF na kuzitumia kwenda nazo Dodoma kuomba ridhaa ya kuchaguliwa nafasi ya Makamu Mwenyeki wa UVCCM

Habari Kubwa