Kesi ya Amber Ruty na wenzake, upelelezi umekamilika

11Feb 2019
Hellen Mwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kesi ya Amber Ruty na wenzake, upelelezi umekamilika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeambiwa kwamba upelelezi umekamilika wa kesi inayomkabili Msanii wa video za wasanii, Rutyfiya Abubakary maarufu kama Amber Ruty na wenzake wawili dhidi ya mashtaka mawili la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Rutyfiya Abubakary maarufu kama Amber Ruty akiingia mahakamani.picha: mtandao

Aidha kesi hiyo itaanza kusikilizwa maelezo ya awali Machi 7, mwaka huu.

Jana kesi hiyo ilipangwa kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Faraja Nguka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Alidai kuwa upande wa Jamhuri unaomba tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Rwizile alisema washtakiwa watasomewa maelezo hayo Machine 7, mwaka huu na dhamana yao inaendelea.

Mbali na Amber Ruty washtakiwa wengine  ni, Saidi Mtopali na James Charles Maarufu kama James Dericious.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa washtakiwa  walifanya mapenzi  kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Ruty, inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya ama baada ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, huku akijua ni kosa kisheria.

Habari Kubwa